11. Kupaa kwa nafsi kwenda mbinguni

9 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Malaika huhudhuria kwa yule anayetaka kukata roho na kama mtu alikuwa mwema husema: ”Toka, ee nafsi nzuri ambayo ilikuwa kwenye kiwiliwili kizuri. Toka ukiwa ni mwenye kusifiwa na pata bishara njema ya rehema, mimea yenye harufu nzuri na Mola si Mwenye kukasirika.” Kutaendelea kusemwa hivo mpaka pale inapotoka. Halafu ipandishwe juu mbinguni. Itaombewa idhini ya kuingia ambapo kutasemwa: “Ni nani huyu?” Kutasemwa kwamba ni fulani ambapo watasema: “Karibu, ee nafsi nzuri iliokuwa kwenye kiwiliwili kizuri. Toka ukiwa ni mwenye kusifiwa na pata bishara njema ya rehema, mimea yenye harufu nzuri na Mola si Mwenye kukasirika.” Hakutoacha kuendelea kusemwa hivo mpaka ifike kwenye mbingu ambayo Allaah (´Azza wa Jall) Yuko juu yake.”

Ameipokea Ahmad katika ”al-Musnad” yake na al-Haakim katika ”al-Mustadrak” ambaye amesema kuwa ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim[1]. Maimamu wengi wameipokea kupitia kwa Ibn Abiy Dhi´b.

[1] Mambo ni kama walivosema. Nimeitaja katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb”(4/188-189).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 85
  • Imechapishwa: 17/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy