19. Mtume akihimiza Sunnah na akitahadharisha Bid´ah

Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Hakika tumeamrishwa kufuata Aathaar zao na kuwafanya kama kiigizo bora kwa kuwaiga. Jengine ni kuwa tumetahadharishwa na mambo yaliyozuliwa na tukaelezwa kwamba ni katika upotevu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]

MAELEZO

Kuwaigiliza katika hayo ni jambo la lazima kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Nzuri na Swahiyh.”

Ameisahihisha al-Albaaniy na wanazuoni wengine.

[1] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidiy (2678), Ahmad (4/126-127), ad-Daarimiy (1/44-45), Ibn Maajah (42-43), al-Haakim (1/95) na wengine. Imaam Ibn Hibbaan, Imaam al-Ajjurriy na Imaam al-Albaaniy (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa ni Swahiyh. Tazama “Swahiyh al-Jaamiy´ as-Swaghiyr” (2/344) ya Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 39
  • Imechapishwa: 14/10/2022