Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Hii ndio njia waliyopita Salaf na maimamu wa Khalaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Wote wamekubaliana kutambua, kupitisha na kuthibitisha sifa zote zilizothibiti katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kuziingilia kwa kuzipindisha maana.

MAELEZO

Mfumo waliopita Salaf kuhusu sifa za Allaah ni kutambua na kuthibitisha zile sifa za Allaah zilizotajwa ndani ya Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kuziingilia kwa kuzipindisha maana kwa mambo yasiyoafikiana na makusudio ya Allaah na Mtume Wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 39
  • Imechapishwa: 14/10/2022