Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa nne

Allaah hasamehi kushirikishwa

Ukishaelewa niliyokwambia na moyo wako umekinaika na ukajua kumshirikisha Allaah ambako Allaah amekuzungumzia kwa kusema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakaye.” (04:48)

MAELEZO

Bi maana ukishaelewa maana ya kihakika ya “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” ya kwamba maana yake ni hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah.

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakaye.”

Wanachuoni (Rahimahu Allaah) wametofautiana juu ya Aayah hii kama inahusiana na shirki zote au ni shirki kubwa peke yake. Kuna waliosema kuwa inahusiana na shirki zote. Hata kama itakuwa ndogo kama kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Allaah hatoisamehe. Wengine wakasema kuwa inahusiana na shirki kubwa peke yake. Aina hii ndio ambayo Allaah hatoisamehe.

Ama kuhusu Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah), wakati fulani anasema maoni hayo ya kwanza na wakati mwingine anasema maoni hayo ya pili.

Kwa hali yoyote ile, ni wajibu kwa mtu kujitenga mbali kabisa na shirki aina zote. Kuna uwezekano mkubwa aina ndogo ikawa inaingia katika ueneaji wa Aayah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 23/04/2022