19- Halafu anasoma al-Faatihah, Aayah moja moja:

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu”, anasimama. Kisha anasema:

الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Sifa zote njema zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu”, anasimama. Kisha anasema:

الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

“Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu”, anasimama. Kisha anasema:

مالك يَوْمِ الدِّينِ

“Mfalme wa siku ya Malipo”, anasimama. Kisha anasema:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunayekuabudu na na Wewe pekee ndiye tunakutaka msaada”, anasimama.

Kisha akiendelea kuisoma namna hiyo. Hivyo ndivyo daima kilivyokuwa kisomo chake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akisimama siku zote mwishoni wa kila Aayah na haiunganishi na Aayah inayofuatia[1].

Wakati mwingine akisoma:

مَلِكِ يَوْمِ الدِّينِ

“Mfalme wa siku ya Malipo.”[2]

[1] Abuu Daawuud na as-Sahmiy (64-65). Imesahihishwa na al-Haakim na adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (343). Abuu ´Amr ad-Daaniy ameipokea katika ”al-Muktafaa” (2/5) na kusema:

“Hadiyth imepokelewa kupitia njia nyingi. Ndio tegemeo katika mlango huu.”

Kisha akasema:

“Imamu wengi waliotangulia na wasomaji wa Qur-aan wamependekeza kusimama katika kila Aayah hata kama baadhi zimefungamana na zingine.”

Sunnah hii wameipa mgongo wasomaji wengi wa Qur-aan, seuze wengine.

[2] ar-Raaziy katika ”al-Fawaa-id”, Ibn Abiy Daawuud katika ”al-Maswaahif” (2/7), Abuu Nu´aym katika ”Akhbaar Aswbahaan” (1/104) na al-Haakim aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Kisomo hiki kimepokelewa kupitia njia nyingi (Mutawaatir) kama kisomo مالك.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 84
  • Imechapishwa: 13/10/2016