18. Kisomo baada ya du´aa za kufungulia swalah na kabla ya al-Faatihah

18- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba kinga kwa Allaah kutokamana na shaytwaan na akisema:

أَعُوذُ باللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيم منْ هَمْزِهِ نَفْخِهِ وَنَفْثِهِ

“Ninajilinda kwa Allaah na shaytwaan aliyefukuzwa na kutokamana na wazimu wake[1], jeuri yake na ushairi wake.”[2]

Wakati mwingine alikuwa akiweza kuongeza na kusema:

أَعوذ بالله السميع العليم من الشَّيْطانِ الرَّجِيمِ من هَمْزِهِ ونَفْخِهِ ونَفثِه

“Ninajilinda kwa Allaah, Mwenye kusikia, Mjuzi, kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa; upilizaji wake, jeuri yake na ushairi wake.”[3]

Baada ya hapo anasoma:

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”[4]

[1] Tafsiri za maneno yote haya imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa isnadi Swahiyh lakini hata hivyo iliyokatika mlolongo wake baina ya Taabi´iy na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Makusudio ya shairi ni shairi lililosemwa vibaya, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika katika mashairi kuna hekima.” (al-Bukhaari)

[2] Abuu Daawuud, Ibn Maajah, ad-Daaraqutwniy na al-Haakim aliyeisahihisha pamoja na Ibn Hibbaan na adh-Dhahabiy. Imetajwa pamoja na upokezi wenye kufuata katika ”al-Irwaa’” (342

[3] Abuu Daawuud na at-Tirmidhiy kwa isnadi nzuri. Maoni haya yana Ahmad, kama ilvyotajwa katika ”al-Masaa-il” (1/50) ya Ibn Haani.

[4] al-Bukhaariy, Muslim, Abuu ´Awaanah, at-Twahaawiy na Ahmad.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 84
  • Imechapishwa: 13/10/2016