19. Inapaswa kuepuka Bid´ah zote

Kama ambavo Bid´ah zinahusiana na mambo ya ´ibaadah zinahusiana vilevile na mambo ya ada na zina jukumu kubwa katika somo letu hili na mimi nitazungumzia mada katika muqtadha wa utangulizi kwa ajili kuingia katika mada yenyewe. Baada ya hapo nitabainisha ulazima wa kujihadhari wa kutumbukia ndani ya Bid´ahkwa ujumla katika mambo ya ´ibaadah au ya ada.

Bid´ah ni kila kitu kinachoachwa au kinachofanywa kwa nia ya kumuabudu Allaah (Ta´ala) kwa njia ambayo haiko katika dini. Hii ndio maana iliyochaguliwa na ash-Shaatwibiy (Rahimahu Allaah) ambaye amesema:

Bid´ah ni njia iliyozuliwa ndani ya dini inayofanana na Shari´ah na inakusudiwa kutekelezwa kwa njia iliyowekwa katika Shari´ah.”[1]

Kama ambavo maana hii inajumuisha mambo ya kidini basi vivyo hivyo juu ya yale mambo ya kiada. Hata hivyo mambo ya kaida yanajumuishwa hapa ikiwa yanahusiana na ´ibaadah na si kwa njia ya kuachia, kitu ambacho ndio sahihi.

[1] al-I´tiswaam (1/51).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 26
  • Imechapishwa: 09/05/2023