19. Hadiyth “Wape bishara njema watembeaji gizani… “

315 – Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

بَشِّرِ المشَّائين في الظُّلَم إلى المساجد بالنّورِ التامِّ يومَ القيامةِ

“Wape bishara njema watembeaji[1] gizani kwenda misikitini kwamba watakuwa na nuru kamili siku ya Qiyaamah.”[2]

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni geni.”

Wapokezi wa cheni ya wapokezi wake ni waaminifu.

316 – Ibn Maajah pia ameipokea kupitia kwa Anas[3].

[1] Makusudio ni wale ambao mara nyingi wana mazowea ya kufanya hivo, na si yule ambaye imetokea akaenda mara kadhaa. Hadiyht inakusudia Fajr na ´ishaa pale ambapo ndio kunakuwa na giza.

[2] Swahiyh kupitia zingine.

[3] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/246)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy