Imekuja katika Hadiyth:

“Du´aa ndio kiini cha ´ibaadah.”

Katika matamshi mengine imekuja:

“Du´aa ndio ´ibaadah.”

Allaah (Subhaanah) amesema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚإِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ

“Mola wenu amesema: “Niombeni Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu, wataingika Motoni wadhalilike.”” (40:60)

Allaah ameiita ´ibaadah kuwa ni du´aa pale aliposema:

إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي

“Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu.”

Bi maana na kuniomba.

Du´aa ni mja kumdhalilikia Allaah na kumuomba na kumtaka uokozi na riziki. Yote haya ni ´ibaadah. Akimfanyia nayo sanamu, mti, mawe au maiti, aliyefanya hayo anakuwa ni mshirikina. Kwa hiyo ni wajibu kutahadhari na shirki aina zote, kubwa na ndogo, na ´ibaadah afanyiwe Allaah pekee.

Lakini hata hivyo haina neno kumuomba mtu ambaye yuko hai na ni muweza kwa kitu anachoweza kukifanya. Sio shirki. Ukimuomba ndugu yako akusaidie kukata mti au kuchimba kisima, hakuna neno. Allaah (Subhaanah) amesema kuhusu kisa cha Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

“Akamsaidia yule ambaye ni katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake.” (28:15)

Mwana wa Israaiyl alimtaka msaada dhidi ya mavamizi. Kwa kuwa Muusa alikuwa anaweza kumsaidia kwa sababu alikuwa anazungumza na kusikia.

Ama kumuelekea kiumbe kwa kitu asichokiweza yeyote isipokuwa Allaah na kuamini kuwa kinanufaisha au kudhuru kwa sababu zisizokuwa za kihisia ni shirki. Ni mamoja kiumbe hichi kiwe hai, hakipo mbele yako au kimeshakufa. Allaah (Ta´ala) amesema kuwa wamesema:

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao hawawezi kuwadhuru na wala hawawezi kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

Wanadhania kuwa wakiwaabudu wanaweza kuwanufaisha kwa kuwaombea mbele ya Allaah ili waweze kufikia malengo yao au kuwakurubisha kwa Allaah. Allaah (Subhaanah) amesema kuwa wamesema:

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.” (39:03)

Hili linathibitisha upotevu na ujinga wao juu ya muombezi na yule mwenye kuombewa. Allaah ndiye mwenye maombezi yote. Yeye ndiye anawaendesha waja Wake vile anavyotaka. Haridhii kuombewa isipokuwa yule ambaye ameridhia matendo yake. Hakuna yeyote awezae kuombea mbele Yake isipokuwa baada ya idhini Yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ

“Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake.” (02:255)

وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ

“HaaHawamuombei uombezi yeyote isipokuwa kwa yule ambaye Amemridhia.” (21:28)

Uombezi hauwi isipokuwa mpaka amuidhinishe yule muombezi na amridhie yule mwenye kuombewa. Hakika (Subhaanah) haridhii isipokuwa tu wapwekeshaji. Imesihi ya kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nani aliye na furaha zaidi atayepata sehemu ya uombezi wako, ee Mtume wa Allaah?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni yule atayesema “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” hali ya kuwa ni msafi ndani ya moyo.””[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Uombezi hautoidhinishwa isipokuwa tu kwa wale waumini wapwekeshaji ambao Allaah ameridhia maneno na matendo yao.

[1] al-Bukhaariy (99).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 29-31
  • Imechapishwa: 10/12/2016