19. Damu ya ugonjwa ilioambatana na hedhi isiyojulikana na upambanuzi usiokuwa salama

Ya tatu: Mwanamke kutokuwa na hedhi yenye kujulikana na upambanuzi uliosalama. Kwa maana ya kwamba damu yake ya ugonjwa inakuwa ni yenye kuendelea tangu pale anapopata damu yake ya kwanza kwa sifa moja au kwa sifa zenye kutofautiana kwa kiasi cha kwamba haiwezi kuwa hedhi. Hapa atafanya kama wanavofanya wanawake wengi. Bi maana atafanya hedhi yake ni siku sita au saba kwa mwezi. Inaanza pale anapoanza kupata damu. Nyingine yote ni damu ya ugonjwa.

Mfano wa hilo apate damu siku ya tano katika mwezi. Damu hiyo iendelee kutiririka na wakati huo huo hawezi kuona upambanuzi wa wazi wenye kuashiria kuwa ni damu ya hedhi. Hakuna chenye kusaidia si rangi wala sifa nyingine. Katika hali hii hedhi yake itakuwa siku sita au saba na inaanza tangu siku ya tano katika kila mwezi. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya Himnah bint Jahsh (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Ee Mtume wa Allaah! Mimi nina damu ya ugonjwa kubwa na yenye nguvu. Unasemaje juu yake? Imenizuia kuswali na kufunga.” Mtume akasema: “Chukua pamba na weka kwenye tupu. Inaondosha damu.” Akasema: “Ni zaidi ya hivyo.”

Katika Hadiyth hiyo hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

Hakika haya ni masumbufu ya shaytwaan. Una hedhi siku sita au saba kwa mujibu wa ujuzi wa Allaah (Ta´ala). Kisha oga. Pale utakapoona umetwaharika kabisa swali siku ishirini na nne au ishirini na tatu na ufunge siku ishirini na nne au ishirini na tatu.”

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh. Imenukuliwa kutoka kwa Ahmad kwamba amesema kuwa ni Swahiyh wakati al-Bukhaariy amesema kuwa ni nzuri.

Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “siku sita au saba” hamaanishi kufanya khiyari bali vile atavyoonelea kuwa ndio karibu na usawa. Ataidurusu hali yake na kuchagua lile analoona kuwa ni lenye kuafikiana bora zaidi na wanawake wenye kufanana naye kwa njia ya kimaumbile, miaka na chimbuko, kile ambacho katika damu yake kimekaribia damu ya hedhi na mambo mengine yenye uwezekano. Akiona kuwa kilicho karibu ni siku sita, afanye kuwa siku sita, na akiona kilicho karibu ni siku saba, afanye kuwa ni siku saba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016