Washirikina na wakanamungu wamepinga kufufuliwa kutokana na akili yao:
وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ
“Walikuwa wakisema: “Je, hivi tutakapokufa na kuwa udongo na mifupa hivi sisi hakika tutafufuliwa au na baba zetu waliotangulia?”[1]
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌٌ
“Akatupigia mfano akasahau kuumbwa kwake; akasema: “Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshasagika na kuwa kama vumbi.”[2]
Allaah (´Azza wa Jall) ametaja dalili nyingi za kiakili zinazofahamisha jambo la kufufuliwa na akasema:
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ
”Naye ndiye aliyeanzisha uumbaji, kisha anaurudisha, nayo ni mepesi mno Kwake.”[3]
Huku ni kwa njia ya kupigia mfano. Ambaye amewaumba kutokana na maji dhalili, hawezi kuwaumba tena kutokana na udongo kama walivyokuwa?
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ
”Je, anadhani mtu ataachwa bure? Hivi hakuwa tone kutokana na manii yanayomwagwa kwa nguvu, kisha akawa pande la damu, akamuumba na akamsawazisha, akamfanya namna mbili; mwanamme na mwanamke? Je, Huyo hakuwa ni muweza wa kuhuisha wafu?”[4]
Miongoni mwa dalili ni kwamba Allaah anaiteremshia mvua ardhi kavu na tasa kisha baada ya masiku machache inageuka kijani kibichi. Je, ambaye anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake hawezi kumuumba tena mtu? Hiki ni kitu kinachoingia akili na chenye kuhisiwa.
وَآيَةٌ لَّهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ
“Na alama kwao ni ardhi iliyokufa, Tukaihuisha na tukatoa humo nafaka, wakapata kuzila.”[5]
Allaah anaihuisha ardhi iliokufa na hivyo inakuwa kijani kibichi.
وَتَرَى الْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنبَتَتْ مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ
“Na utaona ardhi kame, lakini tunapoiteremshia maji hutikisika na kuumuka, na inaotesha mimea ya kila namna, mizuri yakupendeza.”[6]
[1]56:47-48
[2]36:78
[3]30:27
[4]75:36-40
[5]36:33
[6]22:5
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 199
- Imechapishwa: 19/01/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 199
Imechapishwa: 19/01/2025
https://firqatunnajia.com/183-mvua-ni-dalili-tosha-juu-ya-kufufuliwa/