18. Ni nani wa kwanza kuamini ujumbe wa Mtume?

Swali 18: Ni nani wa kwanza kuamini ujumbe wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Wa kwanza kumwamini katika wanawake alikuwa Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

Wa kwanza kumwamini katika wazee alikuwa ni Waraqah bin Nawfal.

Wa kwanza kumwamini katika watu wa kati na kati alikuwa ni Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh).

Wa kwanza kumwamini katika watoto alikuwa ni ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh).

Wa kwanza kumwamini katika watumwa walioachwa huru alikuwa ni Zayd bin al-Haarithah (Radhiya Allaahu ´anh).

Wa kwanza kumwamini katika watumwa alikuwa ni Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh).

Ambao waliingia katika Uislamu kupitia ulinganizi wa Abu Bakr alikuwa ni ´Uthmaan bin ´Affaan, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, Sa´d, Sa´iyd, Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah na wengineo.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 96
  • Imechapishwa: 14/09/2023