18. Nadharia tatu za kizushi kuhusu uumbaji wa Qur-aan

Watu wa Bid´ah katika masuala haya wamegawanyika makundi matatu:

1- Kundi lililosema kwamba Qur-aan imeumbwa. Kama mfano wa Mu´tazilah na wale waliokubaliana nao katika Bid´ah hii mbaya.

2- Kundi lililosema kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa. Kwa mtazamo wa Salaf hawa ni wazushi kama walivowahukumu ukafiri wale waliosema kwamba Qur-aan imeumbwa.

3- Kundi ambalo halisemi kuwa Qur-aan imeumbwa wala haikuumbwa. Hawa ni wale wenye kusimama na kunyamaza na ni waovu zaidi kuliko wale wenye kusema kwamba Qur-aan imeumbwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 101
  • Imechapishwa: 09/04/2019