18. Kuhifadhi maeneo msikitini kwa kuweka viatu au mkeka

Swali 18: Baadhi ya watu wanahifadhi maeneo ndani ya msikiti siku ya ijumaa ilihali wako katika majumba yao. Je, kufanya hivi ni sawa[1]?

Jibu: Hili halijuzu. Kilichowekwa katika Shari´ah ni mswaliji yeye mwenyewe atangulie msikitini kwa ajili ya kuketi maeneo hapo hali ya kusubiri swalah ya ijumaa baada ya yeye kuswali kile ambacho Allaah amemwandikia. Baada ya hapo ajishughulishe na kisomo cha Qur-aan, kusema “Subhaan Allaah”, “Alhamdulillaah”, “Allaahu Akbar”, “Laa ilaaha illa Allaah” na kuomba du´aa mpaka pale atakapotoka imamu.

Kuhusu yale yanayofanywa na baadhi ya watu kwa kuhifadhi maeneo kwa kuweka viatu, kanzu au kitu kingine na wakaondoka, ni jambo lisilofaa. Msikiti ni kwa yule aliyetangulia kufika. Vivyo hivyo safu ya kwanza na ya baada yake ni kwa ajili ya wale waliotangulia kufika. Ambaye amefika kabla ndiye ana haki zaidi. Haifai akahifadhi maeneo kwa kuweka kiatu, zulia au kitu kingine.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/406-407).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 58
  • Imechapishwa: 27/11/2021