5 – Kuyafanya kwa kupangilia

Kinachokusudiwa ni kupangilia viungo vya wudhuu´. Mtu aanze kwa kuosha uso, kisha mikono miwili, kisha afute kichwa halafu aoshe miguu miwili. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُؤُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ

“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni kwa [kupaka maji] vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni.”[1]

Allaah amesema kwa kupangilia. Hakufanywi ufaswaha wa namna hii isipokuwa ni kutokana na faida. Hatuoni faida nyingine katika mazingira haya isipokuwa ni kupangilia. Hivyo ikajulisha kwamba ni jambo la lazima.

[1] 05:06

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 30
  • Imechapishwa: 14/12/2021