Swali: Ni du´aa ipi inayotakiwa kusomwa wakati wa kukata swawm? Mtu afungue swawm kwa kitu gani?

Jibu: Du´aa inayotakiwa kusomwa wakati wa kukata swawm:

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ

“Kiu kimeondoka, mishipa imerowana na ujira umepatikana – Allaah akitaka.”[1]

Mfungaji atafungua kwa tende tosa au tende za kawaida. Akikosa basi atafungua kwa maji, hivyo ndivo katukhabarisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Abu Daawuud (2357), al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (4/239) na katika ”as-Sunan as-Sughraa” (1390) na ad-Daaraqutwniy (240). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl”.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 22
  • Imechapishwa: 21/03/2022