Swali: Kuna du´aa gani iliyopendekezwa wakati wa kukata swawm? Mtu aseme:

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ

“Kiu kimeondoka, mishipa imerowana na ujira umepatikana – Allaah akitaka.”[1]?

Jibu: Imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipokata swawm:

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ

“Kiu kimeondoka, mishipa imerowana na ujira umepatikana – Allaah akitaka.”

Kumepokelewa vilevile:

اللَّهُمَّ لَكَ صُمْتُ وَعَلَى رِزْقِكَ أَفْطَرْتُ

“Ee Allaah! Nimefunga kwa ajili yako na nimefutari kwa riziki yako.”[2]

Kwa hali yoyote kuna uwezekano mkubwa wa kuitikiwa du´aa wakati wa kukata swawm. Kwa hiyo muislamu anatakiwa kuangalia du´aa zenye manufaa na zenye kuenea na aombe kwazo kwa kutaraji kuitikiwa na kupata thawabu za Allaah.

[1] Abu Daawuud (2357), al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (4/239) na katika ”as-Sunan as-Sughraa” (1390) na ad-Daaraqutwniy (240). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl”.

[2] Abu Daawuud (2358), ad-Daaraqutwniy (240) na Ibn-us-Sunniy katika ”´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (482). Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Haikuthibiti.” (Zaad-ul-Ma´aad (2/51))

Ibn Hajar amesema:

”Cheni ya wapokezi ni dhaifu.” (Talkhiysw-ul-Habiyr)

Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan al-Albaaniy” (2358).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 22
  • Imechapishwa: 21/03/2022