Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
136 – Tunawaamini waandishi watukufu. Allaah amewafanya ni wenye kutuhifadhi.
MAELEZO
Kuamini Malaika (´alayhimus-Salaam) ni moja katika nguzo za imani na misingi hii imetajwa ndani ya Qur-aan:
لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ
“Si wema pekee kwa nyinyi kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, lakini wema khaswa ni yule mwenye kumuamini Allaah na siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii.”[1]
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ
”Mtume ameamini yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini; wote wamemuamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Mitume Yake.”[2]
Tunawaamini Malaika na kwamba ni viumbe miongoni mwa viumbe vya Allaah na kwamba ni walimwengu wasioonekana, kwamba hatuwaoni na kwamba Allaah amewaumba kutokamana na nuru. Allaah amewapa kazi ambazo wanazisimamia. Kila mmoja anayo kazi anayoisimamia. Licha ya hivyo wanamwabudu Allaah (´Azza wa Jall) na hawachoki:
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ
“Na ni Vyake pekee vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi na wale walio Kwake hawatakabari na ‘ibaadah Yake na wala hawachoki. Wanasabihi usiku na mchana wala hawazembei.”[3]
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ
“Na wakasema: “Mwingi wa rehema Amejifanyia mwana.” Utakasifu ni Wake! Bali [hao Malaika] ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii kwa kauli nao kwa amri Yake wanafanya.”[4]
Wako sampuli nyingi. Miongoni mwao kuna wanaohifadhi. Nao ni wale ambao Allaah amewapa kazi ya kuwachunga wanadamu na kuyadhibiti matendo yao. Kila mtu anao Malaika wanne wanaomchunga usiku na mchana. Malaika mmoja yuko upande wa kuliani mwake, Malaika mwingine yuko kushotoni mwake. Yule aliyeko upande wa kulia anaandika matendo yake mema, yule aliyeko upande wa kushoto anaandika matendo yake mabaya:
إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ
“Pale wanapopokea wapokeaji wawili wanaokaa kuliani na kushotoni. Hatamki maneno yoyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha [kurekodi].”[5]
Malaika wengine wawili wako mbele yake ambao wanamuhifadhi na mashambulizi maadamu Allaah anawaruhusu kufanya hivo:
لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ
“Ana Malaika wanaofuatana kwa zamu mbele yake na nyuma yake wanamhifadhi kwa amri ya Allaah.”[6]
Wanamlinda kutokamana na mambo ya khatari. Unapofika wakati, wanamwacha na hapo ndipo anafikwa na yale ambayo Allaah amemwandikia. Sisi tunayaamini haya. Tukifanya hivo basi tunatakiwa pia kuona haya kutokama na Malaika watukufu na hivyo tusifanye matendo mabaya na tusizungumze mambo ya batili, kwa sababu wanaandika kila kitu juu yetu.
[1] 2:177
[2] 2:285
[3] 21:19-20
[4] 21:26-27
[5] 50:17-18
[6] 13:11
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 191-192
- Imechapishwa: 09/12/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 191-192
Imechapishwa: 09/12/2024
https://firqatunnajia.com/176-waandishi-watukufu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)