Ni nani anayepanga na kuongoza vita? Ni kiongozi. Sisi tunatakiwa kumfata imamu. Akituamrisha kupambana basi tunatakiwa kupambana na hatupambani pasi na idhini ya kiongozi. Ni kitu kisichojuzu. Ni miongoni mwa kazi zinazomuhusu kiongozi:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ

“Enyi walioamini! Mna nini mnapoambiwa tokeni [mwende kwenye Jihaad] katika njia ya Allaah, mnajitia uzito katika ardhi.”[1]

Vita ni miongoni mwa kazi za kiongozi. Pindi kiongozi atapowateua watu kutoka kwenda kupigana vita basi ni lazima atoke kila ambaye anaweza kubeba silaha.

Haikushurutishwa kwa kiongozi ambaye anasimamia hajj na jihaad awe si mtenda madhambi. Anaweza kuwa na baadhi ya maasi na mambo yanayoenda kinyume. Lakini midhali madhambi yake hayajamfanya kutoka nje ya Uislamu basi ni lazima kupambana jihaad na kuhiji pamoja naye. Wema na nguvu zake ni kwa ajili ya manufaa ya waislamu na kuharibika kwake kunamwangalia yeye. Jihaad na hajj ni kwa ajili ya manufaa ya waislamu. Vivyo hivyo swalah. Tunakuwa naye pale anapopatia na tunajiepusha na makosa yake anapokosea. Hata hivyo hatumfanyii uasi na kusababisha mfarakano. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Manufaa ya waislamu yanasimama juu ya jambo hilo.

Kuhusu Ahl-ul-Bid´ah na wapotofu wanaona kufaa kuwafanyia uasi watawala. Hii ndio ´Aqiydah ya waislamu. Tunajilinda kwa Allaah kutokamana na ´Aqiydah hiyo.

[1] 09:38

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 190-191
  • Imechapishwa: 09/12/2024