75- ´Aqiydah ya Salaf ndio ya sawa kwa mujibu wa dalili za wazi na hoja zenye kuridhiwa katika Qur-aan, Sunnah, maafikiano na akili. Ama katika Qur-aan ni maneno Yake (Ta´ala):
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا
“Yeye ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu, humo mna Aayaat zilizo wazi kabisa – nazondio msingi wa Kitabu – na nyinginezo haziko wazi. Ama wale ambao nyoyoni mwao mna upotevu hutafuta zile zisizokuwa wazi kwa lengo la kutaka fitina na kutaka kuzipotosha. Hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Wale wenye msingi madhubuti katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Mola wetu.”
Amewasema vibaya wale wanaotaka kufasiri zile Aayah zisizokuwa wazi na akawataja sambamba na akawataja pamoja na wale watu wanaotaka mfarakano na fitina. Kisha (Ta´ala) akaeleza kwamba hakuna ajuaye maana yake isipokuwa Allaah pekee. Kwa mujibu wa wanachuoni wengi wanasoma na kusimama katika maneno Yake:
إِلَّا اللَّـهُ
“… isipokuwa Allaah.”
Si sahihi kuwachanganya wanachuoni pamoja na wale wanaojua tafsiri yazo kwa sababu zifuatazo:
1- Allaah amewasema vibaya wale wanaopekua tafsiri yazo. Wanachuoni wangelikuwa wanajua tafsiri yazo basi wale wenye kupekua tafsiri yazo wangelisifiwa na sio kusemwa vibaya.
2- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mkiwaona wale wanaofuata [yale maandiko] yasiyokuwa wazi basi hao ndio wale Allaah alikuwa akielezea. Hivyo tahadharini nao.”[1]
Bi maana, wale wote wanaofuata yale maandiko yasiyokuwa wazi basi hao ndio wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi. Iwapo wanachuoni wangelikuwa ni wenye kujua tafsiri yazo basi kwa kule kuzifuata kwao wangelikuwa ni wenye kusemwa vibaya na wapindaji. Lakini Aayah inawasifu na kupambanua kati ya wao na wale ambao nyoyoni mwao mna upindaji. Hivyo ingelikuwa ni kujigonga.
3- Aayah inafahamisha kuwa tu wamegawanyika mafungu mawili, kwa sababu Amesema:
فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ
“Ama wale ambao nyoyoni mwao mna upotevu… “
Bi maana wako watu ambao nyoyoni mwao mna upindaji ambao wanafuata zile Aayah zisizokuwa wazi na watu walio na elimu yenye kubobea. Kuanzia hapa ni wajibu kila fungu liwe ni lenye kutofautiana na lingine. Kwa msemo mwingine ni kwamba wale ambao elimu zao ni zenye kubobea wametofautiana na wale wapotevu kwa kule kuacha kwao kufuata zile Aayah zisizokuwa wazi maana yake na huku wanasema:
آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا
“Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Mola wetu.”
Wanaacha kupekua zile Aayah zisizokuwa wazi. Hivyo maana ya Aayah inakuwa sahihi. Yule mwenye kuwachanganya wanachuoni katika maana hii hawapambanui wao na wala hawatofautishi na wale waliosemwa vibaya. Kwa hivyo uelewa huu sio sahihi.
4- Kama angelitaka kuwaingiza na kuwachanganya katika tafsiri basi Allaah angelisema:
“… na husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Mola wetu.”
kwa sababu taqdiri ya tafsiri ingelikuwa:
وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا
“Wale wenye msingi madhubuti katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Mola wetu.”
5- Maneno yao:
آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا
“Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Mola wetu.”[2]
yanaonyesha ishara ya kujisalimisha na kumwachia Allaah yale wasiyoyajua, kwa sababu ni yenye kutoka kwa Allaah kama ambavyo yale yaliyo wazi pia ni yenye kutoka kwa Allaah.
6- Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) pindi walipokuwa wanamuona ambaye anafuata na kuuliza juu ya yale maandiko yasiyokuwa wazi basi wangelikuwa wakimzingatia kuwa amepinda. Hivyo ndivyo ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alivomuona Swabiygh ambapo akamchapa na kumfunga na akawaamrisha watu wajitenge naye. Kisha baadaye Swabiygh akakiri juu ya uoni wa mbali wa ´Umar ambapo akatubu na akaacha kufanya yale aliyokuwa akifanya. Akanufaika kwa kufanyiwa hivo na akasalimika kutofanya uasi pamoja na Khawaarij. Kitu kama hicho kisingeliwezekana endapo ile tafsiri na maana ya ndani ingelikuwa ni yenye kutambulika.
7- Lau kama tafsiri ingelikuwa ni yenye kufahamika kwa wale wanachuoni waliobobea kielimu basi maana yake ni kwamba wasingelikuwepo wengine wenye kuifahamu zaidi yao. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amekanusha kwamba hakuna mwingine aliye na elimu hiyo. Hivyo haitojuzu kwa mwingine kujipatia elimu hiyo isipokuwa yule ambaye itathibiti kwamba ni katika wanachuoni waliobobea, jambo ambalo linapelekea kwamba imeharamishwa kwa wale watu wa kawaida na wanafunzi mpaka pale watapofikia ile elimu iliobobea. Mvutano katika jambo hili unafanya kwamba inafaa kwa kila mmoja kufasiri kwa sababu Aayah imekhalifu hali zote mbili.
[1] al-Bukhaariy (4547) na Muslim (2665).
[2] 03:07
- Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 35-37
- Imechapishwa: 19/12/2018

Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 35-37
Imechapishwa: 19/12/2018
https://firqatunnajia.com/17-salaf-walikuwa-ni-wenye-kupatia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)