17. Sababu ya kumi na sita ya maisha mazuri: Maneno ya watu dhidi yako hayakudhuru chochote, bali yanawadhuru wao

16- Miongoni mwa mambo yenye manufaa ni kwamba unatakiwa utambue kuwa maudhi ya watu juu yako na khaswa katika kuzungumza maneno mabaya hayakudhuru wewe na bali yanawadhuru wao. Isipokuwa pale ambapo utaishughulisha nafsi yako kuyatilia umuhimu na ukaiwezesha kumiliki zile hisia zako. Katika hali hiyo ndipo zitakudhuru wewe kama zilivyowadhuru wao. Lakini maadamu wewe hutoyapa umuhimu basi hayatokudhuru chochote.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 29
  • Imechapishwa: 29/06/2020