16. Sababu ya kumi na tano ya maisha mazuri: Linganisha kati ya neema na baya lililomtokea au linalowezea kumtokea

15- Anatakiwa pia pindi anapopatwa na jambo baya au akalichelea basi alinganishe kati ya neema zilizobaki alizonazo za kidini na za kidunia na yale mambo ya kuchukiza yatayokuwa yamempata. Wakati wa kulinganisha ndio atabainikiwa na ule wingi wa neema alizo ndani yake na kuyumbikayumbika yale mambo mabaya yaliyompata. Vivyo hivyo alinganishe yale madhara anayochelea kumzukia na yale mengi yawezayo kumtokea katika kusalimika nayo. Kwa hiyo asiache uwezekano ambao ni dhaifu ukashinda mawezekano mengi yenye nguvu zaidi. Kwa njia hiyo itaondoka misononeko na khofu yake na pia akadirie ule uwezekano mkubwa zaidi unaoweza kumpata na aiandae nafsi yake endapo litamtokezea na afanye bidii kukizuia kile ambacho hakijamtokezea na kukiondosha au kukipunguza kile ambacho tayari kimekwishamtokea.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 29
  • Imechapishwa: 29/06/2020