Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kumepokelewa [Hadiyth] Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kupambana na viongozi madhalimu muda wa kuwa wanaswali[1].

MAELEZO

Viongozi – ijapo watakandamizi na wakadhulumu – muda wa kuwa watalazimiana na Uislamu haifai kuwapiga vita. Wanatakiwa kunasihiwa. Ama wakifanya ukafiri wa wazi ni lazima kuwapiga vita kwa yule mwenye uwezo. Ikiwepo nguvu na uwezo basi watu watafanya hivo. Vinginevyo itakuwa si lazima.

[1] Muslim (1854).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 03/11/2020