18. Inahusiana na kuhuisha na kufufua kilichopo na sio kuzusha

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Jariyr bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa kuna mtu aliyetoa swadaqah na watu wakawa wamemuigiliza. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Yule mwenye kuweka katika Uislamu msingi mzuri basi ana ujira wake na ujira wa yule atakayeifanya baada yake pasi na kupungua chochote katika ujira wao. Na yule mwenye kuweka katika Uislamu msingi mbaya basi ana madhambi yake na madhambi ya yule atakayeifanya pasi na kupungua chochote katika madhambi yao.”[1]

Ameipokea Muslim ambaye amepokea tena mfano wa Hadiyth kama hiyo kupitia kwa Abu Hurayrah:

“Yule mwenye kuita katika uongofu…”

na

“Yule mwenye kuita katika upotevu…”[2]

MAELEZO

Yule mwenye kuweka… – Bi maana mwenye kuhuisha na kudhihirisha Sunnah na si uzushi. Msingi wa Hadiyth ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaona watu mafukara. Alipoona ufukara wao ndipo akawakhutubia watu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawahimiza kutoa swadaqah na akawapendezea nayo na kusema:

”Mtu anaweza kutoa swadaqah ya dinari, dirhamu, nguo, ngano hata kipande cha tende.” Mtu mmoja kutoka Answaar akaja na mfuko ambao ulikaribia kumshinda kuubeba. Watu wakaanza kuleta baada yake mpaka nikaona matuta mawili ya chakula na nguo. Uso wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukanawiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Yule mwenye kuweka katika Uislamu msingi mzuri basi ana ujira wake na ujira wa yule atakayeifanya baada yake… ”

[1] Muslim (1017).

[2] Muslim (2674).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 03/11/2020