Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Khawaarij:

“Popote mnapokutana nao basi waueni. Ikiwa nitakutana nao basi nitawaua kama walivyouawa kina ´Aad.”[1]

MAELEZO

Popote mnapokutana nao… – Kutokana na ukubwa wa Bid´ah yao. Kwa sababu waliwababaisha  watu ambapo wakafanya bidii katika usomaji wa Qur-aan na swalah mpaka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Mmoja wenu ataidharau swalah yake akilinganisha na swalah yao na kisomo chao akilinganisha na kisomo chake.”

Wakawasafiri namna hiyo waislamu na hivyo wakawapiga vita. Kutokana na ujasiri wao mbaya wakampiga vita mwenye kutenda dhambi ikiwa ni pamoja na kumpiga vita ´Aliy, ´Amr bin Khaarijah na jopo kubwa. Yote hayo kutokana na uzushi na upotevu wao. Hali iliendelea hivo mpaka pale Allaah alipomsaidia ´Aliy akawapiga vita. Khawaarij ni wenye shari kubwa. Wanaona kuwa wako katika haki katika kuwaua watenda madhambi, viongozi na raia. Yote haya ni kutokana na ujinga na upotevu wao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Popote mnapokutana nao basi waueni. Kwani hakika katika kuwaua kuna ujira kwa mwenye kufanya hivo siku ya Qiyaamah.”

“Ikiwa nitakutana nao basi nitawaua kama walivyouawa kina ´Aad.”

[1] al-Bukhaariy (3611) na Muslim (1066).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 03/11/2020