17. Washirikina walikuwa wanajua Shahaadah ina maana gani

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Makusudio ya maneno haya ni maana yake na sio kuyatamka peke yake. Makafiri wajinga walijua makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) kwa neno hili ni kumpwekesha Allaah (Ta´ala) kwa ´ibaadah na kukanusha vinavyoabudiwa badala Yake na kujitenga navyo mbali kabisa. Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaambia: “Semeni: “Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah””, wakasema:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ

“Amewafanya miungu wote hawa kuwa mungu Mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno!” (38:05-07)

MAELEZO

Nayo ni maneno “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah”.

Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):

“Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaambia… “

Sentesi hii ni kama ile ilio kabla yake, anabainisha (Rahimahu Allaah) ya kwamba “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” maana yake ni hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Anabainisha ya kwamba washirikina walilielewa hili na walijua kuwa makusudio sio kule kutamka peke yake. Walitambua kuwa maana yake ni hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Kwa ajili hii waliikanusha, pamoja na kwamba hawakuwa wakipinga ya kwamba Allaah peke Yake ndiye Muumbaji na Mwenye kuruzuku.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 23/04/2022