Masuala matatu – Kujifunza maana yake hapa ni kusoma kwa wanachuoni, kuhifadhi na kufahamu. Huku ndio kusoma. Makusudio sio mtu kujisomea kivyake. Huku sio kusoma. Kusoma ni kule mtu kupokea kutoka kwa wanachuoni na wakati huohuo mtu akayahifadhi hayo na akayafahamu kikamilifu. Huku ndio kusoma kwa njia sahihi. Ama mtu kujisomea kivyake peke yake hakutoshi katika kujifunza. Ingawa ni jambo linalotakikana na lenye faida lakini halitoshi mtu akaishilia kwa hilo.

Haijuzu kwa kujifunza kutoka katika vitabu, kama ilivyo hii leo. Kwa sababu kujifunza kutoka katika vitabu ni jambo lina khatari sana. Ndani yake kunatokea madhara na mwenye kusoma anapata madhara makubwa kuliko mjinga. Kwa sababu mjinga ananijua kuwa ni mjinga na anasimama kwenye mpaka wake. Lakini anayejifanya amesoma anajiona kuwa ni msomi na hivyo matokeo yake anahalalisha vile alivyoharamisha Allaah, anarahamisha vile alivyohalalisha Allaah, anazungumza na kumsemea Allaah pasi na elimu. Masuala haya yana khatari kubwa.

Elimu haichukuliwi moja kwa moja kutoka katika vitabu. Vitabu ni njia. Kuhusu uhakika wa elimu inachukuliwa kutoka kwa wanachuoni; kizazi kimoja inakipokeza kizazi kingine. Vitabu ni njia ya kujifunza elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 42
  • Imechapishwa: 26/11/2020