Katika Aayah moja imekuja:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ
“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye Mlinzi wa wale walioamini na kwamba makafiri hawana mlinzi.”[1]
Katika Aayah nyingine imekuja:
ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ
”Kisha watarudishwa kwa Allaah Mola wao wa haki.”[2]
Wanahoji ni vipi hili litakuwa katika maneno yaliyo wazi? Hivyo wakaitilia shaka Qur-aan.
Ama Aayah:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ
“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye Mlinzi wa wale walioamini na kwamba makafiri hawana mlinzi.”
maana yake ni kwamba Allaah ni Mnusuraji wa waumini, lakini makafiri hawana mwenye kuwanusuru.
Kuhusu Aayah:
ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ
”Kisha watarudishwa kwa Allaah Mola wao wa haki.”
kunamaanishwa duniani ambapo kuna waungu wengi wa batili. Haya ndio yale waliyoyatilia shaka mazanadiki[3].
[1] 47:11
[2] 6:62
[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:
”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))
Ibn Taymiyyah amesema:
”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.” (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)
Ibn Kathiyr amesema:
”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))
Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:
”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 84-85
- Imechapishwa: 16/04/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)