Wanasema kuwa Allaah kwenye Aayah moja anasema:

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

”Hakika Allaah anapenda waadilifu.”[1]

Katika Aayah nyingine imekuja:

وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا

”Ama wale waliopotoka na njia ya haki, basi hao watakuwa ni kuni za Motoni!”[2]

Wanauliza yatakuweje haya katika maneno yaliyo wazi.

Ama Aayah:

وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا

”Ama wale waliopotoka na njia ya haki, basi hao watakuwa ni kuni za Motoni!”

inahusiana na wale watu wanaowalinganisha viumbe wengine na Allaah na badala yake wakawaabudu wao pasi na Allaah.

Kuhusu Aayah:

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

”Hakika Allaah anapenda waadilifu.”

Allaah anawaamrisha watu wafanye uadilifu kati yao, kwa sababu Allaah anawapenda wale wafanyao uadilifu. Amesema katika Aayah nyingine:

أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ

”Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Bali wao ni watu wanaolinganisha!”[3]

Bi maana wanashirikisha. Hii ndio tafsiri ya yale waliyoyatilia mashaka mazanadiki[4].

[1] 5:42

[2] 72:15

[3] 27:60

[4] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 16/04/2024