Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

12- Msimamizi wa kila kitu Asiyelala.

MAELEZO

Amejisimamia Mwenyewe na amewasimamia wengine wote. Amejisimamia Mwenyewe na hahitajii chochote. Yeye ni mkwasi wa yeyote na chochote. Amewasimamia wengine wote. Kila kitu ni chenye kumuhitajia na kila kitu kinahitajia kusimamiwa Naye (Subhaanahu wa Ta´ala). Lau Allaah asingelisimamia mbingu, ardhi na viumbe vyengine vyote, basi vingeliharibika na kuangamia. Lakini hata hivyo Allaah anavisimamia, anavihifadhi na kuvitunza kwa yale yanayowafaa. Kila kiumbe ni chenye kumuhitajia Yeye:

إِنَّ اللَّـهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ

“Hakika Allaah anazuia mbingu na ardhi zisitoweke na zikitoweka, basi hakuna yeyote wa kuzishikilia baada Yake.”[1]

[1] 35:41

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 12/09/2019