Swali: Mtu wa kawaida ambaye anawanyamazia makafiri ilihali ni muweza wa kukemea.

Jibu: Huyu anahesabika ni mtenda dhambi. Mwenye kufanya hivo ameidhulumu nafsi yake. Lakini hakufuru isipokuwa akiafikiana nao kwa maneno, matendo au kimoyo katika moja katika mambo haya matatu. Akinyamazia jambo ambalo ni wajibu kwake – nalo ni kukemea maovu – anazingatiwa ni mtenda dhambi kwa kunyamaza kwake. Kwa sababu anaweza kufanya na hakufanya. Pengine anaogopa. Kinacholengwa ni kwamba ni lazima kwake kukemea maovu. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[1]

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Mmekuwa Ummah bora kabisa ulioteuliwa kwa watu: mnaamrisha mema na mnakataza maovu.”[2]

Swali: Je, kunyamaza hakuzingatiwi ni kuridhia ukafiri?

Jibu: Hapana, sio kuridhia ukafiri. Haipelekei huko.

[1] 09:71

[2] 03:110

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 135
  • Imechapishwa: 12/09/2019