33 – Qays bin Hafsw ametuhadithia: ´Abdul-Waahid ametuhadithia: al-Hasan bin ´Amr al-Fuqaymiy ametuhadithia: Mujaahid ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdullaah bin ´Amr akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anayeunga sio mwenye kulipiza wema. Lakini muungaji ni yule ambaye, wakati kizazi kinapokatwa basi yeye anakiunga.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 130
  • Imechapishwa: 08/01/2025