17- Yahyaa bin ´Ammaar al-Imaam ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Adiy ametuhadithia: Haatim bin Mahbuub ametuhadithia: ´Abdul-Jabbaar ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah: ´Abdullaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Pindi mtu anaposema:
بسم الله
“Kwa jina la Allaah… “
Wakati mwingine alisema:
“Pindi mtu anaposema:
سُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلَا حَوْلَوَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ وَتَبَارَكَ اللَّهُ
“Ametakasika Allaah, himdi zote anastahiki Yeye, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni mkubwa, hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa uwezo wa Allaah na amebarikika Allaah.”
anaipokea Malaika na kuiweka chini ya mbawa zake mpaka inapofika kwenye uso wa Mola wa walimwengu (Tabaarak wa Ta´ala).”
Wakati mwingine alisema:
“… anaipokea Malaika na kuiandika… “
- Muhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 43
- Imechapishwa: 21/01/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket