Sharti la kusihi swawm ya Sunnah mchana ni kutofanya kitu kinachovunja swawm kabla ya kuweka nia, kama vile kula, kunywa au kujamiana. Ikiwa mtu atafanya lolote kati ya haya baada ya alfajiri, basi swawm yake haitasihi kwa sababu amefanya kichenguzi baada ya alfajiri.

Maalikiyyah, Daawuud adh-Dhwaahiriyyah, Ibn Hazm na al-Muzaniy – ambaye naye ni katika ash-Shaafi’iyyah – wameona kuwa kuweka nia kabla ya alfajiri ni sharti ya kusihi swawm ya Sunnah. Swan’aaniy pia ameegemea maoni haya[1]. Wanatumia hoja kwa ueneaji wa Hadiyth iliyotangulia:

“Yule asiyelaza nia kabla ya alfajiri hana swawm.”[2]

Ibn Hazm alijibu kuhusu Hadiyth ya mlango huu kwa kusema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka nia ya kufunga kabla ya alfajiri pale aliposema:

“Hakika nimeamka nimefunga.”

Alipokosa chakula ndipo akaendelea na swawm yake. Kisha alipoelezwa kuwepo kwa chakula akala.

Maoni ya kwanza ndiyo yenye nguvu zaidi kutokana na Hadiyth zilizotangulia. Aidha ni maoni yaliyopokelewa kutoka kwa Maswahabah waliotajwa na al-Bukhaariy. Isitoshe Ibn Hazm amepokea maoni yao kuwa walikuwa wakifunga kwa kuweka nia mchana. Nao wana ujuzi mkubwa zaidi juu ya Qur-aan na makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuliko sisi. Jengine ni kwamba upokezi wa al-Bayhaqiy kutoka kwa ´Aaishah uliyotangulia unasema:

“Basi mimi nimefunga.”

Hii karibu iwe dhahiri kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga kwa nia ya mchana.

[1] “al-Umm” (02/35), “al-Hidaayah” (01/119), “al-Mughniy” (06/340), “al-Majmuu’” (06/302) na “Subul-us-Salaam” (02/304).

[2] Ahmad (6/287), Abu Daawuud (2454), at-Tirmidhiy (730), an-Nasaa’iy (2331), Ibn Maajah (1700) na Ibn Khuzaymah (1933).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/23-24)
  • Imechapishwa: 05/02/2025