Hata hivyo wanazuoni wametofautiana kuhusu ni wakati gani mchana nia inawekwa. Imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas, Ibn ´Umar, Anas na Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba mpaka katikati ya mchana ndiyo ukomo wa kuweka nia na kwamba si sahihi nia kuwekwa baada ya hapo. Hayo pia ndio maoni ya Abu Haniyfah na wafuasi wake[1]. ash-Shaafi’iy katika maoni ya pili na Ahmad wanasema kwamba swawm ya Sunnah inasihi kuweka nia ya mchana hata baada ya katikati ya mchana, kwa sababu maandiko yanafahamisha kufaa kuweka nia kuanzia mchana hayakubainisha tofauti kati ya nia kabla au baada ya katikati ya mchana. Wanazuoni wametofautiana tena: Je, mtu anapata thawabu ya siku nzima au anapata thawabu kuanzia wakati aliweka nia tu? Wanazuoni wametoa juu ya maoni mawili:
1 – Mtu hatapata thawabu isipokuwa kuanzia wakati aliweka nia tu. haya ndio maoni ya Shaafi’iyyah na Hanaabilah[2]. Hilo ni kutokana na kauli maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”
Huyu hakuweka nia ya swawm isipokuwa baada ya kupita sehemu ya mchana. Kwa hivyo hatapata thawabu isipokuwa kwa kiwango alichonuia.
2 – Analipwa thawabu mchana mzima. Hayo ni maoni ya Hanafiyyah na baadhi ya wanazuoni wa Hanaabilah[3], kwa sababu amejizuilia mchana wote na amechelewesha nia.
Hata hivyo maoni ya kwanza ndio yenye nguvu kwa mujibu wa dalili. Maoni ya pili yako karibu zaidi na usawa inapokuja katika upana wa fadhilah za Allaah – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] “Muswannaf” ya Ibn Abiy Shaybah” (03/28).
[2] “al-Mughniy” (6/342), uk. 193.
[3] ”Fath-ul-Qadiyr” (2/312), “al-Hidaayah” ya Abu al-Khattwaab (02/51) na “al-Inswaaf” (03/298).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/24)
- Imechapishwa: 05/02/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/24)
Imechapishwa: 05/02/2025
https://firqatunnajia.com/17-wakati-gani-nia-inayowekwa-mchana-na-thawabu-zake/