16. Sababu ya kumi na mbili ya talaka ambayo ni maisha ya anasa aliyokulia mke nyumbani kwao

12 – Maisha ya anasa aliyoibukia mwanamke

Maisha ya anasa ambayo mwanamke amekulia nyumbani kwa baba yake. Amelelewa juu ya anasa na starehe ambapo akiwa na dada wa kazi, akiwa na dereva, akiwa na nyumba ya wasaa, akiwa na chumba chake cha kulala cha kujitegemea na kadhalika. Anapokuja katika nyumba ya mume hana dereva, dada wa kazi na nyumba yake ni ya kawaida. Busati ya chakula iko juu ya ardhi ilihali yeye mwanamke alikuwa akila juu ya meza na hivi sasa yeye ndiye anahudumu. Hali imembadilikia. Ikiwa hakuandaliwa maisha haya, basi maisha ya anasa aliyokulia juu yake yatabaki kwenye kumbukumbu na akili yake na anayataka lakini hayapati. Hapo ndipo hupendelea kuendelea kuishi nyumbani kwa baba yake pasi na kujali ataishi katika hali gani, kwa sababu hana uvumilivu baada ya anasa zilizopita. Hii ni sababu miongoni mwa sababu za talaka. Ni mambo yanayotokea katika maisha yetu, yameshuhudiwa na yanatutesa sana katika baadhi ya jamii.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 12/04/2024