Kwa hakika walikuwa wakionelea “mungu” ni yule ambaye anakusudiwa kwa ajili ya mambo haya; ni mamoja ikiwa ni Malaika, Mtume, walii, mti, kaburi au jini. Hawamaanishi ya kwamba mungu huyu anaumba, kuruzuku na kuendesha mambo. Kwa hakika wao walikuwa wanajua kuwa [mwenye uwezo wa] hayo ni Allaah pekee, kama tulivyotangulia kusema. Isipokuwa wanachomaanisha kwa neno “mungu” ni kama wanavyomaanisha washirikina wa zama zetu kwa neno “bwana”. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawajilia kuwalingania katika Tawhiyd; ambayo ni hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.
MAELEZO
Hapa anachotaka (Rahimahu Allaah) ni kubainisha kuwa washirikina walikuwa hawamaanishi kwamba hakuna mwenye kuyaendesha mambo wala mwenye kuumba isipokuwa Allaah. Walikuwa wakijua kuwa hayo ni haki. Wao walikuwa wakipinga maana ya hakuna muabudiwa mwengine wa haki isipokuwa Allaah. Sababu ya mtunzi kuanza [kitabu] namna hii na kukariri ni kutaka kutilia mkazo na kumraddi yule mwenye kusema kuwa yeye anawaabudu Malaika au wengine, kwa sababu tu wamkurubishe mbele ya Allaah na sio kwa sababu anaonelea kuwa wanaumba au kuruzuku.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kash-is-Shubuhaat, uk. 40-41
- Imechapishwa: 07/10/2023
Kwa hakika walikuwa wakionelea “mungu” ni yule ambaye anakusudiwa kwa ajili ya mambo haya; ni mamoja ikiwa ni Malaika, Mtume, walii, mti, kaburi au jini. Hawamaanishi ya kwamba mungu huyu anaumba, kuruzuku na kuendesha mambo. Kwa hakika wao walikuwa wanajua kuwa [mwenye uwezo wa] hayo ni Allaah pekee, kama tulivyotangulia kusema. Isipokuwa wanachomaanisha kwa neno “mungu” ni kama wanavyomaanisha washirikina wa zama zetu kwa neno “bwana”. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawajilia kuwalingania katika Tawhiyd; ambayo ni hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.
MAELEZO
Hapa anachotaka (Rahimahu Allaah) ni kubainisha kuwa washirikina walikuwa hawamaanishi kwamba hakuna mwenye kuyaendesha mambo wala mwenye kuumba isipokuwa Allaah. Walikuwa wakijua kuwa hayo ni haki. Wao walikuwa wakipinga maana ya hakuna muabudiwa mwengine wa haki isipokuwa Allaah. Sababu ya mtunzi kuanza [kitabu] namna hii na kukariri ni kutaka kutilia mkazo na kumraddi yule mwenye kusema kuwa yeye anawaabudu Malaika au wengine, kwa sababu tu wamkurubishe mbele ya Allaah na sio kwa sababu anaonelea kuwa wanaumba au kuruzuku.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kash-is-Shubuhaat, uk. 40-41
Imechapishwa: 07/10/2023
https://firqatunnajia.com/16-mlango-wa-03-yule-mwenye-kuwaomba-uombezi-wengine-anatambua-kuwa-allaah-ndiye-mola/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)