16. Mke mwema halaani na hakufuru wema

10 – Mwenye kuacha kulaani. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kuelekea katika uwanja wa kuswali [swalah ya] Dhuhaa´ au [swalah ya] al-Fitwr kwenda kwa wanawake na kusema:

“Enyi kongamano la wanawake! Toeni swadaqah. Kwani hakika mimi nyinyi ndio wakazi wengi wa Motoni.” Tukasema: “Kwa nini, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Mnakithirisha laana na mnakufuru wema.”[1]

[1] al-Bukhaariy (01/405 ), (03/325), (04/191) na (05/266 – Fath), Muslim (889) na wengineo.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 28/09/2022