15. Mke mwema haombi talaka pasi na sababu ya kimsingi

9 – Hamuombi mume wake talaka pasi na sababu yenye kumpelekea kufanya hivo. Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote atakayemuomba mume wake talaka pasi na sababu, basi ni haramu kwake harufu ya Pepo.”[1]

[1] Abu Daawuud (2226), at-Tirmidhiy (1187) ambaye ameifanya kuwa ni nzuri, ad-Daarimiy (02/162), Ibn Maajah (2055) na wengineo. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy kwa mujibu wa sharti za Muslim katika “al-Irwaa´” (07/100).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 28/09/2022