14. Mke mwema hamuidhinishi yeyote kuingia nyumbani bila idhini ya mume

8 – Asimpe idhini yeyote kuingia nyumbani kwa mume wake isipokuwa kwa idhini yake. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke kufunga na mume wake hakusafiri pasi na idhini yake, asimpe idhini nyumbani kwake[1] isipokuwa kwa idhini yake na chochote anachokitoa pasi na amri yake basi na mume atapata nusu yake.”[2]

[1] Asimpe idhini yeyote kuingia nyumbani kwake au kula humo isipokuwa kwa idhini yake.

[2] al-Bukhaariy (09/16 – Fath), Muslim (1026) na wengineo.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 31
  • Imechapishwa: 28/09/2022