16. Kukata masharubu, kucha na nywele za sehemu ya siri za maiti

Swali 16: Je, inafaa kukata masharubu, nywele za kwapa, kucha na nywele za sehemu ya siri za maiti[1]?

Jibu: Imependekezwa kupunguza masharubu na kukata kucha zake. Kuhusu kunyoa nywele za sehemu ya siri na nywele za kwapani sijui kinachofahamisha juu uwekwaji Shari´ah wa mambo hayo. Bora ni kutofanya hivo. Kwa sababu ni kitu kilichojificha na si chenye kuonekana kama kucha na masharubu.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/111-112).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 20
  • Imechapishwa: 13/12/2021