15. Ni lazima wakati wa kumuosha maiti kutumia mkunazi?

Swali 15: Je, katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas[1] kuna dalili inayojulisha ulazima wa kutumia mkunazi?

Jibu: Ni kitu kilichowekwa katika Shari´ah. Wanazuoni wanaona kuwa imependekezwa. Kwa sababu inatakasa zaidi. Ikiwa haitokuwa wepesi mkunazi basi kufanywe badala yake sabuni au Ashnaan[2] au vinavyoweza kukaa mahala pake.

[1] Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla ´alayhi wa sallam) amesema juu ya yule ambaye ameanguka kutoka katika kipando chake akafa:

”Muosheni kwa maji na mkunazi na mumkafini katika nguo zake.”

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake. Kitaab-ul-Janaaiz kutoka katika ”Buluugh-ul-Maraam” Hadiyth nambari. 564.

[2] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Saltwort

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 19
  • Imechapishwa: 13/12/2021