Hishaam ad-Dastawaa-iy amesimulia kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Hilaal bin Abiy Maymuunah, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa Rifaa´ah al-Juhaniy, aliyehadithia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

”Kunapopita nusu ya usiku, au theluthi yake, basi Allaah (´Azza wa Jall) anashuka katika mbingu ya chini na kusema mpaka kupambazuke: ”Siulizi juu ya waja Wangu mwengine isipokuwa Mimi Mwenyewe. “Nani anayeniomba msamehe Nimsamehe? Ni nani anayeniomba Nimuitikie? Ni nani anayeniomba Nimpe?”[1]

Abu Muhammad al-Makhladiy ametukhabarisha: Abul-´Abbaas as-Sarraaj ametukhabarisha: Muhammad bin Yahyaa ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Muusa ametuhadithia: kutoka kwa Israa’iyl, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr, aliyesema: Nashuhudia ya kuwa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah ya kwamba wameshuhudia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (´Azza wa Jall) hutoa muhula mpaka kupite theluthi ya kwanza ya usiku.  Hapo ndipo anashuka katika mbingu ya chini na akasema mpaka kupambazuke: ”Je, kuna mwenye dhambi? Je, kuna mwenye kuomba msamaha? Kuna mwenye kuomba? Je, kuna mwenye kuuliza? Kuna mwenye kuomba du´aa?”[2]

Abu Muhammad al-Makhladiy ametukhabarisha: Abbul-´Abbaas ath-Thaqafiy ametukhabarisha: al-Hasan bin as-Sabaah ametukhabarisha: Shabaabah bin Sawwaar ametuhadithia, kutoka kwa Yuunus bin Abiy Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr, aliyesema: Nashuhudia ya kuwa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah ya kwamba wameshuhudia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (´Azza wa Jall) hutoa muhula mpaka kupite theluthi ya usiku hapo ndipo anashuka katika mbingu hii. Kisha huamrisha ikafunguliwa milango ya mbingu na kusema: ”Je, kuna mwenye kuomba Nimpe? Je, kuna mwenye kuomba Nimjibu? Je, kuna mwenye kuomba msamaha Nimsamehe? Je, kuna mwenye kudhikika Nimwondoshee matatizo Yake? Je, kuna mwenye kuomba msaada Nimsaidie?” Huendelea kubaki maeneo hayo mpaka kukapambazuka alfajiri, katika kila usiku wa dunia.”

Abu Muhammad al-Makhladiy ametukhabarisha: Abul-´Abbaas (ath-Thaqafiy) ametukhabarisha: Mujaahid bin Muusa na al-Fadhwl bin Sahl ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Shariyk ametuhadithia: kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa al-Agharr, aliyeshuhudia ya kwamba Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd ya kwamba wameshuhudia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wakati kunapopita theluthi ya usiku, basi Anashuka (Tabaarak wa Ta´ala) katika mbingu ya dunia na akasema: ”Je, kuna mwenye kuomba msamaha Nimsamehe? Je, kuna mwenye kuomba Nimpe maombi yake? Je, kuna mwenye kutubu Nimkubalie tawbah yake?”

[1] Ahmad (4/16).

[2] ash-Shariy´ah, uk. 310, ya al-Aajurriy.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 216-220
  • Imechapishwa: 10/12/2023