16. Hii ndio njia wanayofuata Ahl-us-Sunnah al-Jamaa´ah

Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah… – Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa yale waliyokuja nayo Mitume kwa sababu ndio Njia ilinyooka. Njia hiyo ni kumpwekesha Allaah, kumtii, kuamini majina na sifa Zake na kwamba Yeye hana anayeshabihiana Naye, hana anayelingana Naye na wala hana mshirika (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio njia iliyonyooka. Njia ambayo Allaah amesema juu yake:

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ

“Tuongoze njia iliyonyooka.” (02:06)

Njia hiyo ni:

الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ

“Wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli na mashuhadaa na waja wema.” (04:69)

Njia yao ni kumuamini Allaah na majina na sifa Zake na wakati huo huo mtu amtakase Allaah kufanana na viumbe Wake na badala yake amsifu kwa sifa kamilifu, kutii maamrisho Yake, kujiepisha makatazo Yake na kusimama katika mipaka Yake. Hii ndio njia iliyonyooka. Njia hiyo ni ile:

الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ

“Wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli na Mashuhadaa na waja wema.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com