366 – al-Haarith, mtumwa wa ´Uthmaan aliyeachwa huru, ameeleza:

“Siku moja ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) alikaa chini na sisi tukakaa naye. Akaja muadhini ambapo akaitisha maji ndani ya chombo. Nadhani ndani yake kunaingia viganja viwili vilivyojazwa vya mikono. Akatawadha kisha akasema: “Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha mfano wa kutawadha kwangu huku. Halafu akasema:

“Yule atakayetawadha kutawadha kwangu huku kisha akasimama kuswali swalah ya Dhuhr, basi atasamehewa yale yaliyokuwa kati yake na Subh. Wakati ataposwali ´Aswr, basi atasamehewa yale yaliyokuwa kati yake na Dhuhr. Wakati ataposwali Maghrib, basi atasamehewa yale yaliyokuwa kati yake na ´Aswr. Wakati ataposwali ´Ishaa, basi atasamehewa yale yaliyokuwa kati yake na Maghrib. Halafu pengine akalala na akijigeuzageuza katika usiku wake. Iwapo atasimama, akatawadha na kuswali Subh, basi atasamehewa yale yaliyokuwa kati yake na ´Ishaa. Nazo:

الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ

”… mema yanaondosha maovu .”[1]

Wakasema: “Hayo ni matendo mema. Ni yepi mema yenye kubakia, ee ´Uthmaan?” Akasema: “Ni:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ و سُبْحَانَ اللَّهِ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, Allaahu ni Mkubwa, hapana matikisiko wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”[2]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri, Abu Ya´laa na al-Bazzaar.

[1] 11:114

[2] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/269-270)
  • Imechapishwa: 24/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy