Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ

”… hawatokuwa na chakula isipokuwa kutokana na kichaka chenye miba, chenye kunuka na mchungu mno.”

Kisha akasema:

إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ طَعَامُ الْأَثِيمِ

”Hakika mti utakaomezwa kwa ukali, ni chakula cha mtenda dhambi nyingi.”[1]

Hapa anathibitisha chakula kingine. Hivyo wakaitilia mashaka Qur-aan na wakadai kuwa ni yenye kujigonga.

Ama Aayah:

لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ

”… hawatokuwa na chakula isipokuwa kutokana na kichaka chenye miba, chenye kunuka na mchungu mno.”

maana yake ni kwamba hawana chakula kingine katika mlango huo isipokuwa kichaka chenye miba, chenye kunuka na mchungu mno. Mti huo utaliwa katika mlango mwingine. Hiyo ndio maana ya maneno Yake:

إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ طَعَامُ الْأَثِيمِ

”Hakika mti utakaomezwa kwa ukali, ni chakula cha mtenda dhambi nyingi.”

Hii ndio tafsiri ya yale waliyoyatilia mashaka mazanadiki[2].

[1] 44:43-44

[2] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 83-84
  • Imechapishwa: 15/04/2024