Amesema:

أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ

“Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa!”[1]

Katika Aayah nyingine amesema:

فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ

”… lakini atakayekufuru katika nyinyi baada ya hapo, basi hakika Nitamwadhibu adhabu ambayo Sitomwadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.”[2]

Katika Aayah ya tatu amesema:

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ

“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika Moto.”[3]

Wakaitilia mashaka Qur-aan na wakasema kuwa ni yenye kujigonga.

Kuhusu maneno Yake:

أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ

“Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa!”[4]

kunamaanishwa adhabu ya ule mlango ambao wako ndani yake.

Ama Aayah:

فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ

”… lakini atakayekufuru katika nyinyi baada ya hapo, basi hakika Nitamwadhibu adhabu ambayo Sitomwadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.”

inahusiana na kwamba Allaah aliwageuza nguruwe, akawaadhibu kwa kuwageuza maumbile jambo ambalo kamwe hajapatapo kulifanya kwa watu wengine.

Kuhusu Aayah:

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ

“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika Moto.”

Moto una milango saba kwa majina Jahannam, Ladhwaa, Hutwamah, Saqar, Sa´iyr, Jahiym na Haawiyah. Wanafiki watakuwa katika matabaka ya chini kabisa[5].

[1] 40:46

[2] 5:115

[3] 4:145

[4] 40:46

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 15/04/2024