Muusa amesema:

سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ

“Utakasifu ni Wako! Nimetubu Kwako nami ni wa kwanza wa wanaoamini.”[1]

Wachawi wakasema:

إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ

”Hakika sisi tunatumai kwamba Mola wetu atusamehe madhambi yetu kwa vile tumekuwa wa kwanza wenye kuamini.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

“Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni muislamu wa kwanza.”[3]

Wanauliza atawezaje Muusa kusema kuwa yeye ndiye muumini wa kwanza ilihali hapo kabla Ibraahiym, Ya´quub na Ishaaq walikuwa waumini kabla yake. Itakuweje Muusa na wachawi waseme hivo? Itakuweje Mtume aseme namna hiyo ilihali kabla yake walikuweko waislamu wengi wakiishi kabla yake, kama vile ´Iysaa na wafuasi wake? Hivyo wakaitilia mashaka Qur-aan na wakaituhumu kuwa ni yenye kujigonga.

Muusa alisema hivo pale ambapo alisema:

رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي

”Mola wake akamsemesha, [Muusa] alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” Akasema: “Hutoniona.””[4]

Hakuna yeyote anayemuona Allaah duniani isipokuwa atakufa:

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ

”Mola wako alipojidhihirisha katika jabali akalifanya livurugike kuwa vumbi na Muusa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Utakasifu ni Wako! Nimetubu Kwako nami ni wa kwanza wa wanaoamini.””[5]

Bi maana wa kwanza wenye kukusadikisha ya kwamba hakuna yeyote atakayekuona duniani isipokuwa atakufa.

Wachawi wamesema:

إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ

”Hakika sisi tunatumai kwamba Mola wetu atusamehe madhambi yetu kwa vile tumekuwa wa kwanza wenye kuamini.”

Bi maana wakopti wa kwanza wa kimisri wenye kumsadikisha Muusa.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ

”… nami ni wa kwanza wa wanaoamini.”

Bi maana katika watu wa Makkah. Hii ndio tafsiri ya yale waliyoyatilia mashaka mazanadiki[6].

[1] 7:143

[2] 26:51

[3] 6:162-163

[4] 7:143

[5] 7:143

[6] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 79-81
  • Imechapishwa: 15/04/2024