Swali: Tunaomba utubainishie baadhi ya adabu za funga zilizopendekezwa?

Jibu: Miongoni mwa adabu za funga zilizopendekezwa ni kuchelewesha daku kwa njia ya kwamba mtu amalize kula punde kidogo kabla ya kuchomoza alfajiri ya pili. Nyingine ni kuharakisha kukata swawm. Miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa vilevile ni kumtaja Allaah, kusoma Qur-aan na matendo mengine mbalimbali ya kheri. Adabu kubwa zaidi ni kuhifadhi swalah ya Tarawiyh.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 21
  • Imechapishwa: 24/03/2022