Swali: Ni kwa kitu gani na ni lini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akila daku?

Jibu: Alikuwa akichelewesha daku yake na kitambo kilichokuwa kati ya kuanza kwa daku yake mpaka kukimiwa kwa swalah[1] ni kiasi cha kusoma Aayah 50. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Uzuri ulioje wa tende kama daku ya muumini!”[2]

[1] al-Bukhaariy (575).

[2] Abu Daawuud (2345). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1/621).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 22
  • Imechapishwa: 24/03/2022